Skip to main content

Posts

Mji wa Kisasa Sumbawanga Kuvutia wawekezaji.

Mradi wa upimaji viwanja Nambogo  na Katumba Azimio  umetekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), hii itasaidia upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa na kuwekewa miundombinu ya msingi  na kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi waishio katika kata za pembezoni za Pito, Molo, Milanzi, Lwiche nk.
Jumla ya viwanja 2161 vimepimwa katika eneo hilo la Nambogo na Katumba Azimio kwa matumizi mbalimbali ikiwemo makazi, makazi na biashara, shule, huduma za afya, maofisi, kituo cha biashara (Shopping Mall), vituo vya mafuta, viwanja vya michezo na maeneo ya kupumzikia.
viwango vya matumizi ya viwanja. Na Aina ya matumiziGharama kwa kila mita ya mraba 1Makazi pekee (ujazo wa juu, kati na chini2,700/= 2Makazi na biashara3,000/= 3Biashara5,000/= 4Huduma za jamii3,500/= 5Ibada/ kuabudu3,500/= 6Hoteli, vituo vya mafuta na maduka ya kuiwekezaji5,000/=
 Fomu zitaanza kutolewa mwezi wa 4/2018 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga. wahi sasa…
Recent posts

"Hakuna kidato cha Kwanza atakayebaki nyumbani 2018" Afisa Elimu - Sumba...

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imewahakikishia wananfunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2018 kwamba watapata nafasi ya kuendelea na masomo yao huku Manispaa hiyo ikiendelea na juhudi za kujenga madarasa yanayohitajika.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Sumbawanga Silvester Mwenekitete alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya juhudi za manispaa  kuhakikisha wanapambana na upungufu wa madarasa zaidi ya 18 yanayohitajika ili wanafunzi zaidi ya 2000 waendelee na masomo yao.
Amesema kuwa tayari Manispaa ya Sumbawanga imeagiza tani 90 za sementi kwaajili ya utekelezaji huona baada ya siku saba wanafunzi watakuwa na mahala pa kusomea  ili waweze kutimiza ndoto zao.
"Madarasa yanajengwa katika shule mbalimbali, kizwite Sekondari madara matatu, Sumbawanga Sekondari manne, Katuma, matatu, kila mahali madarasa janajengwa na  tumerekebisha madarasa natayari tuna madarasa ya kutosha, tayari halmashauri imeshaagiza tani 90 za simenti kw…

Wakulima na Wasambazaji mbolea Rukwa Waridhishwa na upatikanaji wa mbolea hadi vijijini.

Wafanyabiashara wakubwa wa mbolea Mkoani Rukwa pamoja na wakulima wameridhishwa na upatikanaji wa mbolea na kusifu juhudi za serikali baada ya kupaza sauti zao na kusikika na Rais Dk. John Pombe Magufuli na jambo hilo kufanyiwa kazi ndani ya muda mfupi.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa wakulima hivi sasa hawapangi tena foleni kusubiri mbolea iliyokuwa ikipatikana kwa taabu na kwa kunyang’anyiana na kuwa foleni hizo zimekwisha na wakulima hawana haja ya kutoka Kijiji kuja mjini kufuata mbolea kwani mbolea hizo zinawafuata huko waliko hasa baada ya marekebisho ya bei elekezi iliyotolewa na Uongozi wa mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
Mmoja wa Wafanyabiashara hao wakubwa Mohamed Rashid Mdangwa wa Kampuni ya ETG amesema “Sasa wakulima wameanza kupata mbolea kwa wingi, mwanzo walikuwa wanapanga foleni hapa lakini kuanzia ile Jumatatu agizo la Rais kuwa mbolea iende Mkoa wa Rukwa, sasa hivi population (wingi) ya watu imepungua sana,  sasa hivi mahitaji ya mbo…

Manispaa ya Sumbawanga yapania kuimarisha huduma ya maji Vijiji kupitia ...

Sumbawanga Dance Sakata 2017

Afisa Utamaduni aunda umoja wa wasanii Sumbawanga

Afisa Utamadunia wa Manispaa ya Sumbwanga Charles Kiheka amepania kuunda umoja wa wasanii wa maigizo katika manispaa ya Sumbawanga baada ya kutana na wasanii hao kwa lengo la kuwaelimisha namna ya kuweza kujisajili ili watambulike kisheria na kuisogeza Sanaa yao nje ya mipaka ya Mkoa nan chi kwa ujumla.

Amelifanya hilo baada ya kuona kuwa wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuwa kazi zao hazithaminiwi na wanunuzi na kukosa ushirikiano kutoka serikalini hivyo kupelekea maisha yao kuendelea kuwa duni licha ya kuipenda kazi wanayoifanya kwakuwa wanajipatia kipato kupitia kazi hiyo.
“Wasanii mmekuwa katika makundi makundi, hamna ushirikiano katika kazi zenu, kila mtu ameonekana kujua kuliko mwengine, hampeani nafasi, hamshauriani kwa mwendo huu hatuwezi kufika na kama tutafanya kazi kwa ushirikiano tutakuwa mfano wa kuigwa n ahata halmashauri nyingine, Suluhisho pekee mimi nitasimamia uundwaji wa umoja wa wasanii katika Manispaa hii.” Kiheka alisem.
Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Nd…

Sumbawanga yajipanga kwenye Kilimo