Mkurugenzi
wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amesema kuviwezesha vikundi vya
ujasiliamali ni kuzalisha ajira na ubunifu kwa vijana na wanawake hao ambao
ndio nguzo ya maendeleo ya mji wa Sumbawanga nan chi kwa ujumla.
![]() |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu |
Ameyasema
hayo alipokuwa akikabidhi hundi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milini 20
kwa vikundi 13 vya wanawake, vikundi 3 vya vijana na kimoja cha walemavu katika mkutano mfupi
uliuofanyika katika ukumbi wa manispaa hiyo mapema mwezi huu.
Amesema
“Nia ya manispaa yetu ni kuongeza kipato kwa wanakikundi, kuinua hali ya maisha
yao, kuboresha hali ya maisha ya kiuchumi ngazi ya kaya pamoja na kuboresha
maisha ya wajasiliamali.”
Comments
Post a Comment