Mkurugenzi wa Manispaa ya
Sumbawanga Jacob Mtalitinya amewasihi vijana wa Manispaa ya Sumbawanga
kujitokeza kwa wingi katika shindano la kutafuta vipaji ili kuitumia fursa hiyo
katika kuviibua na kuviendeleza vipaji vyao huku wakiitangaza Manispaa pamoja na
Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
![]() |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya (Kushoto) akipokea “T-Shirt” ya mashindano kutoka kwa Afisa utamaduni wa manispaa hiyo Kiheka Charles (kulia). |
![]() |
Mmoja wa Wasanii wa Sumbawanga akitoa burudani katika mashindano ya “Sumbawanga Talent Search” |
![]() |
Mmoja wa Wasanii wa Sumbawanga akitoa burudani katika mashindano ya “Sumbawanga Talent Search” |
![]() |
Mmoja wa Wasanii wa Sumbawanga akitoa burudani katika mashindano ya “Sumbawanga Talent Search” |
![]() |
Kikundi cha Wasafi Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya “Sumbawanga Talent Search” |
![]() |
Kikundi cha Swax Boys Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya “Sumbawanga Talent Search” |
Amesema kuwa kwa muda mrefu Mkoa wa Rukwa hasa wilaya ya Sumbawanga
imekuwa na sifa ambayo wengi wakiisikia wanakuwa wanatishika hivyo shindano
hili ni fursa ya kuonyesha mambo mazuri yanayopatikana ndani ya mji wa
Sumbawanga na Mkoa. Ametoa wito kwa wananchi, vijana, pamoja na wazazi
kujitokeza na kuwarusu vijana wao kuonyesha vipaji vyao kuvitumia na
kuhakikisha wanajiimarisha siku zijazo kujipatia ajira.
“Idara ya maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Afisa utamaduni tumeona tuwe
na hili shindano ambalo litatumika kuibua vipaji lakini pia kuwaendeleza vijana
ambao tunaaamini wakiendelezwa watatengeneza ajira, kwahiyo kipaji ni ajira,
hivuyo niwasihi sana vijana wa Sumbawanga kutumia nafasi hii kuhakikisha kwamba
wanaendeleza vipaji vyao,” Alisisitiza.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga, Kiheka Charles
amesema kuwa manispaa ya Sumbawanga ina vipaji vingi na nia ya kuanzisha
mashindano hayo ni kutoa muongozo kwa wasanii wenye vipaji mbalimbali kuweza
kuyafikia malengo yao.
“Ofisi ya Mkurugenzi kupitia ofisi ya afisa utamaduni Manispaa ya
Sumbawanga tuliamua kuandaa shindano hili lenye lengo la kuwasaidia vijana
kuitangaza sanaa yao, kukuza vipaji vyao, na kuweza kuitumia sanaa kama chanzo
cha ajira na kunufaika, hivyo basi tunaomba wasanii mbalimbali wenye vipaji
wajitokeze kwa wingi kushiriki,”Alisema.
Halikadhalika, baadhi ya wasanii waliohudhuria kwenye mashindano hayo
waliupongeza uongozi wa halmashauri kwa kuwathamini na kuwajali na kuomuomba
aendelee kuwaibulia vitu vingine ambavyo vitakuwa ni fursa kwa vijana ili
kuweza kuitangaza sumbawanga na Mkoa.
Mmoja wa washiriki wa mashindano hayo Switbert Filbert a.k.a Fire Music
alisema “Tunamshukuru sana Mkurugenzi kwa kuanzisha shindano kama hili na
tunamuomba kama kuna vingine anavifikiria avifanye kwasababu mkoa wa rukwa upo
nyuma katika sanaa, michezo na mengine hivyo tunawaahidi watanzania, wanarukwa
na Sumbawanga kuwa tutafanya vizuri.”
Aidha, mshiriki mwenzie wa mashindano hayo Daniel Benedicto a.k.a Dabeto
alisema “Mashindano haya yakiendelea kwa Mkoa wetu wa Rukwa sana sana
Sumbawanga tunaweza tukatoka sana kwasababu wasanii wengi hawapati muda wa
kuonyesha vitu vyao wazi kama vile kupata fursa ya “ku-perform” mbele za watu,
wengi tulikuwa tunahofu kwamba unaweza kuonyesha sehemu gani, wengi walikuwa
wanjificha ndani, hii ni fursa ya kutengeneza mashabiki.”
Mashindano hayo ya “Sumbawanga Talent Search” yenye kauli mbiu “Kipaji ni
Zawadi Thamini Sanaa Yako” yanasimamiwa na Afisa utamaduni ambaye pia ni msanii
wa “Hip-Hop” aliyedhamiria kushirikiana na Mkurugenzi wa manispaa hiyo kuinua
vipaji vya vijana wa Sumbawanga.
Comments
Post a Comment