WAKATI Serikali inatarajia kuajiri katika sekta ya
afya watumishi wapya 7680 (6180 wa Ofisi ya Tamisemi na 1500 wa Wizara ya
afya), halmashauri nchini zimetakiwa kutumia ripoti za mfumo wa WISN plus POA
iliyorahisishwa kusambaza watumishi wapya kwa kuzingatia uzito wa kazi na
mahitaji kama yalivyoainishwa kwenye taarifa hizo.
Kauli hiyo imetolewa katika kikao kazi kilicholenga
kuwasilisha matokeo ya uchambuzi wa mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo wa
WISN plus POA iliyorahisishwa kinachofanyika mkoani hapa.
Mfumo wa WISN plus POA hutumika kukokotoa mahitaji
ya watumishi kwa kila kada katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia uzito
wa kazi katika kituo husika.
Kwa sasa mfumo huu unatumika kwa ajili ya vituo vya
afya na Zahanati tu, ukijumuisha kada mbalimbali zilizopo katika ngazi hizo za
utoaji huduma ambazo ni waganga (MO), waganga wasaidizi (AMO), tabibu (CO),
tabibu wasaidizi (CA), maafisa wauguzi (NO), maafisa wauguzi wasaidizi (ANO),
na wauguzi (EN).
Kikao kazi hicho pia kilitumika kuzijengea uwezo
Halmashauri na Mikoa ili ziweze kutumia WISN plus POA iliyorahisishwa kusambaza
watumishi wapya, na katika kuomba watumishi wapya.
Akizungumza katika kikao kazi hicho
kilicholenga kuwasilisha matokeo ya zoezi la kubaini mahitaji ya
watumishi kwa kutumia mfumo wa WISN PLUS POA iliyorahishwa Mganga Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam alisema mfumo huo ni toleo jipya unaowezesha
kutumia taarifa kutoka mfumo wa DHIS 2 kwa ajili ya kukokotoa mahitaji ya
watumishi, hivyo kupunguza gharama za kutembelea vituo kwa ajili ya kukusanya
taarifa.
Kikao kazi hicho kilishirikisha Maafisa
Utumishi wa Mikoa na Halmashauri, Waganga wakuu wa wilaya, Makatibu wa Afya wa
Mikoa na Wilaya, Waratibu wa MTUHA wa Halmashauri na Wadau wa Maendeleo wa
Mradi wa PS3.
Mfumo huo ni sehemu ya Mradi wa Uimarishaji wa
Mifumo katika Sekta ya Umma – “Public Sector System Strengthening – (PS3)
unaotekelezwa kwa ufadhili awatu wa Marekani kupitia USAID.
Tayari Halmashauri za mkoa wa lindi,Ruvuma na mtwara zimeshapatiwa mafunzo kwa kanda ya mtwara ikifuatiwa na mikoa ya Tanga na Pwani
mwisho
Na Abdulaziz Ahmeid
Comments
Post a Comment