Walimimu
pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Itwelele wameipongeza Ofisi ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbanga kwa kuweza kukamilisha ujenzi wa maabara ya
Fizikia iliyokuwa hitajio kubwa la shule hiyo ili kutoa wataalamu wa somo hilo.
![]() |
Maabara ya Shule ya Sekondari Itwelele |
Maabara
hiyo iliyokamilika mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu imegharimu shilingi
milioni 45, huku serikali kuu ikichangia shilingi milioni 30, wananchi nao
wakichangia shilingi milioni 10 na Manispaa kuchangia shilingi milioni 5.
Mmoja
wa waalimu wa sayansi katika shule hiyo James Mwambije amesema kuwa ameona nia
ya serikali katika kuhakikisha inatekeleza sera ya Tanzania ya viwanda kwa
kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi ili kuzalisha wataalamu wa
kutosha.
“Dunia
tuliyonayo sasa ya Sayansi na Teknolojia inawahitaji sana wataalamu watakaoweza
‘ku-operate’ (kuendesha) mitambo katika viwanda mbalimbali ambavyo ndio nia ya
serikali yetu, sasa haya mazingira wanayotuwekea ndio hasa yatakayowezesha Tanzania
kufikia ndoto yake,” Alisema.
Kwa upande
wake Hamisi Ulaya akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesifu juhudi za
serikali za kuboresha huduma za elimu bila ya upendeleo na kuongeza kuwa ifike
wakati watu wasione tofauti ya kusoma Dar es salaam na Sumbawanga.
Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imetenga
kiasi cha shilingi 234,656,000/= katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa
ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari 17.
Comments
Post a Comment