Katika kukabiliana na wingi wa
wananfunzi uliotokana na muitikio mkubwa wa sera ya elimu bure Halmashauri ya manispaa
ya Sumbawanga inaendelea na ujenzi wa madarasa matano pamoja na ofisi moja ya
waalimu katika shule ya msingi Kasisiwe.
![]() |
Shule ya Msingi Kasisiwe |
Mradi huo ambao utagharimu shilingi
milioni 67.3 upo katika hatua ya kupiga plasta na tayari shilingi milioni 57.2
zimeshatumika na kutarajiwa kumalizika mwezi mei mwaka huu.
Kaimu Afisa elimu Msingi Manispaa ya
Sumbawanga Frank Sichalwe amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutapunguza
msongamano wa wanafunzi wanaosoma katika shule za Msingi Chanji, Utengule, Ndua
na Kizwite na Milanzi.
” Ujenzi
ukikamilika utapunguza umbali kwa wanafunzi Kwenda shuleni, Wanafunzi na walimu
kujifunza na kufundisha katika mazingira mazuri, Kuongeza tija ya ufaulu kwa
wanafunzi kwa kusoma katika mazingira mazuri,” Alifafanua.
Hadi
kukamilika kwa shule hiyo serikali kuu imechangia shilingi milioni 44.7,
wananchi shilingi milioni 17.3 huku halmashauri ikiwa imechangia shilingi
milioni 5.2.
Comments
Post a Comment