Shilingi Bilioni 1.5 zatumika kuanzisha mji wa kisasa Sumbawanga


Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF) wametumia shilingi bilioni 1.5 kupima viwanja na kuviwekea miundombinu katika eneo la Nambogo mjini Sumbawanga kwa lengo la kuboresha makazi.
Nambogo

Afisa Mipango Miji ardhi na maliasili wa manispaa ya Sumbawanga Thadeo Maganga amesema kuwa mji wa Nambogo utakuwa ni mji wa mfano katika ukanda huu wa ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa katika kupunguza ujenzi holela kwenye miji inayoendelea kama Sumbawanga.

“Kufanikiwa kwa mradi huu utaijengea uwezo manispaa kupanga na kupima maeneo mengine na kuzuia ujenzi holela na msongamano katikati ya mji pamoja na uuzwaji wa viwanja hivi kuiongezea halmashauri mapato,” Alifafanua.

Jumla ya viwanja 2161 vimepimwa katika eneo hilo la Nambogo na Katumba Azimio kwa matumizi mbalimbali ikiwemo makazi, makazi na biashara, shule, huduma za afya, maofisi, kituo cha biashara (Shopping Mall), vituo vya mafuta, viwanja vya michezo na maeneo ya kupumzikia.

Kati ya hivyo Viwanja vyenye ujazo wa juu (HD)    900, Viwanja vyenye ujazo wa kati (MD)   687, Viwanja vyenye ujazo wa chini (LD)    439, Viwanja vyenye ujazo wa chini uliozidi (SLD)   126, Maeneo ya wazi (OS) 9.

viwango vya matumizi ya viwanja.
Na
Aina ya matumizi
Gharama kwa kila mita ya mraba
1
Makazi pekee (ujazo wa juu, kati na chini
2,700/=
2
Makazi na biashara
3,000/=
3
Biashara
5,000/=
4
Huduma za jamii
3,500/=
5
Ibada/ kuabudu
3,500/=
6
Hoteli, vituo vya mafuta na maduka ya kuiwekezaji
5,000/=



Comments