Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid
Njovu amesema kukamilika kwa maabara ya fizikia katika shule ya sekondari
Muhama kutawaandaa wananfunzi wa shule hiyo kutekeleza sera ya viwanda na
kuweza kujiari.
![]() |
Maabara mpya ya Shule ya Sekondari Muhama |
Amesema kuwa wanafunzi hawataweza kufanya
vizuri katika masomo ya sayansi kama hawatawezeshwa kufanya masomo yao kwa
vitendo hali itakayopelekea kutoa wanafunzi mahiri katika masomo hayo na
kuongeza ufaulu.
“Maabara hii ya Sekondari ya Muhama ni kati
ya maabara 9 zilizokamilika ujenzi wake katika Manipaa, tunaamini ukamilifu
wake utaleta ushawishi kwa wanafunzi wa shule hii kupenda masomo ya sayansi
pamoja na kurahisisha ufundishaji wa masomo hayo kwa waalimu,” Alisema.
Kwa upande wake Afisa elimu Sekondari Manispaa
ya Sumbawanga Sylvester Mwenekitete amesema kuwa serikali ilijitahidi kutoa
vifaa vya maabara lakini kwa ukamilifu wa majengo haya kutawezesha kuvihifadhi
vifaa hivyo mahala salama.
Ujenzi huo wa maabara ya Fizikia umegharimu
shilingi milioni 45, huku serikali huu ikiwa imetoa shilingi milioni 30,
wananchi wakiwa wametoa shilingi milioni 13 na halmashauri kuchangia shilingi
milioni 3.
Halmashauri katika kutekeleza agizo la
ujenzi wa maabara tatu kwa kila shule ya sekondari, imefanikiwa kujenga vyumba
vya maabara 51, ambapo vyumba 9 vya maabara vimekamilika na vyumba 42 viko katika hatua mbalimbali ya
ukamilishaji.
Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imetenga
kiasi cha shilingi 234,656,000/= katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa
ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari 17.
Comments
Post a Comment