Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeanzisha
ujenzi wa shule mpya ya msingi katika kata ya Matanga, Wilayani Sumbawanga ili
kukabiliana na wingi wa wananfunzi walioandikishwa katika shule ya msingi
Mtibwa kutokana na sera ya elimu bure iliyoanza mwaka wa masomo 2016.
![]() |
Shule Mpya ya Msingi Mtimbwa, Sumbawanga. |
Shule hiyo mpya itakayoitwa Mtimbwa B tayari
inaendelea na ujenzi wa madarasa saba yatakayogharimu shilingi milioni 75
ambapo hadi sasa milioni 56.6 imeshatumika na kubakia milioni 18.3 ili
kumalizia ujenzi huo ulioanza mwishoni mwa mwaka 2017 na kutegemewa kumalizika
mwaka huu.
Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu
amesema kuwa manispaa imeamua kuanzisha shule hiyo mpya ili kuboresha mazingira
ya wananfunzi na walimu ya kujifunza na kufundishia pamoja na kuongeza tija ya ufaulu
kwa wananfunzi kwa kusoma katika mazingira mazuri.
Akitoa mchanganuo wa fedha za ujenzi wa
madarasa hayo Njovu alisema “Wachangiaji wa ujenzi huu ni serikali kuu amabayo
imechangia 45,300,000 Halmashauri 15,000,000 pamoja na wanachi 14,700,000”
Ujenzi huo wa madarasa saba ya shule mpya ya
msingi Mtimbwa B utapunguza mahitaji ya madarasa 801 yanayohitajika katika Manispaa
ya Sumbawanga ili kuwa na madarasa 1309 yatakayotosheleza wananfunzi wa shule
ya msingi 58,641 katika Manispaa.
Comments
Post a Comment