Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga
Hamid Njovu ameipongeza taasisi ya vijana inayojishughulisha na mazingira Rukwa
Environmental Youth Organization (REYO) katika kuwahamasisha wananchi kupanda
miti ili kutunza mazingira ya manispaa.
![]() |
Kitalu cha miti REYO |
Amesema kuwa ili kuendelea kutunza hali
ya hewa safi iliyopo katika mji wa Sumbawanga kila mmoja ana nafasi ya
kuhakikisha tunafanikiwa kupanda miti mingi iwezekanavyo kwakuwa miti inafaida
nyingi ikiwemo matunda kwaajili ya kuboresha afya, mbao ambazo huitajika
kutengeneza samani ambazo huongeza ajira nchini.
“Nichukue nafasi hii kukipongeza
kikundi cha REYO, wanatusaidia katika kuhakikisha tunafikia malengo ya kupanda
miti milioni 1.5 katika mwaka wa fedha 2017/2018 ambayo ni malengo ya kimkoa
ambapo wao hadi sasa wamegawa bure miche 16,870
katika tasisi za serikali na kuotesha miche 135, 000,” Amesema.
Ameongeza
kuwa kikundi hicho kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 23 Kutoa mafunzo ya uanzishwaji
wa vitalu kwa vitendo kwa vijana 18 ambao wamejiajiri na wanaendelea na kazi
hii katika mkoa wa Rukwa na Katavi.
Katika mwaka wa fedha 2017/2018
maandalizi ya upandaji miti yanaendelea ambapo mpaka sasa Manispaa ya
Sumbawanga ina jumla ya vitalu 24 vya miti vilivyoanzishwa ambavyo vina zaidi
ya miche 980,000 ya matunda na mbao.
Comments
Post a Comment