Manispaa ya Sumbawanga kupitia mradi wa
uboreshsaji miji imetenga kiasi cha shilingi 7,368,573,061 kwaajili ya ujenzi
wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 4.6 itakayounganisha
kata za Majengo, Msua na Chanji.
![]() |
Barabara inayoendelea kujengwa |
Mradi
huo ulioanza mwishoni mwa mwaka 2017 tayari umeshatumia shilingi bilioni 1.6 na
kutegemewa kumalizika mwezi wa 9 mwaka 2018 inayotoka Mwaiseni, kata ya chanji kupitia
Johnkella, kata ya Msua hadi Kanisa la Neema katika kata ya Majengo.
Katika
kuuelezea mradi huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amesema
kuwa ukamilifu wa ujenzi huo utapunguza uharibifu wa vyombo usafiri na
kuboresha muonekano wa mji wa Sumbawanga.
“Hadi
kufikia mwisho wa mwaka tunaamini barabara hii itakuwa imekamilika kulingana na
mkataba uliopo na kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi na
wafanyabiashara katika Mji wa Sumbawanga,” Amesema.
Ujenzi
wa barabara hiyo utachochea shughuli za kiuchumi, ajira na kipato katika
Manispaa ya Sumbawanga na kupunguza msongamano katikati ya mji.
Comments
Post a Comment