Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
imeendelea na ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya Mazwi kilichopatiwa shilingi
milioni 500 na serikali kuu ili kuboresha huduma za afya na kutarajiwa
kuhudumia wananchi 94,856.
![]() |
Kituo cha Afya Mazwi |
Kituo hicho kinachoendelea na ujenzi kimeongeza
majengo ya Maabara, Kichomea taka, Jengo la Mama Baba na Mtoto, Vyoo na Kibanda
cha mlinzi tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya azma ya serikali kuboresha
kituo hicho.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga Dkt.
Archie Hellar ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais. Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kutenga fedha hizo na kuweza kuboresha huduma ya afya
katika manispaa ya Sumbawanga yenye kituo kimoja cha afya kinachomilikiwa na
serikali.
“Kuimarisha
huduma za Afya kwa wananchi kwa kusogeza huduma
karibu kwa zaidi ya Wakazi 94,856 wa Kata ya Mazwi na maeneo mengine
yasiyo za Zahanati wala kituo cha afya ikiwemo Kata za Izia, Momoka , Mafulala,
Msua ,Lwiche na Sumbawanga asilia,”
Amesema.
Ameongeza
kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutawezesha kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuwezesha
watoto wote kupata chanjo kwa wakati ili kuwakinga na magonjwa yanayozuilika
kwa chanjo, pamoja na kuijenga jamii iliyo na watu wenye Afya nzuri na kushiriki katika shughuli mbalimbali za
Maendeleo.
Kwa sasa Halmashauri ina jumla ya vituo
vya tiba 42 ikiwemo Hospitali 2 ya rufaa ya Mkoa na DDH, Vituo vya Afya 3 kimoja
kikiwa cha serikali, na zahanati 35, 20 zikiwa za serikali.
Comments
Post a Comment