Mji wa Kisasa Sumbawanga Kuvutia wawekezaji.


Mradi wa upimaji viwanja Nambogo  na Katumba Azimio  umetekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), hii itasaidia upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa na kuwekewa miundombinu ya msingi  na kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi waishio katika kata za pembezoni za Pito, Molo, Milanzi, Lwiche nk.

Jumla ya viwanja 2161 vimepimwa katika eneo hilo la Nambogo na Katumba Azimio kwa matumizi mbalimbali ikiwemo makazi, makazi na biashara, shule, huduma za afya, maofisi, kituo cha biashara (Shopping Mall), vituo vya mafuta, viwanja vya michezo na maeneo ya kupumzikia.

viwango vya matumizi ya viwanja.
Na Aina ya matumizi Gharama kwa kila mita ya mraba
1 Makazi pekee (ujazo wa juu, kati na chini 2,700/=
2 Makazi na biashara 3,000/=
3 Biashara 5,000/=
4 Huduma za jamii 3,500/=
5 Ibada/ kuabudu 3,500/=
6 Hoteli, vituo vya mafuta na maduka ya kuiwekezaji 5,000/=

 Fomu zitaanza kutolewa mwezi wa 4/2018 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga. wahi sasa 

Comments