"Hakuna kidato cha Kwanza atakayebaki nyumbani 2018" Afisa Elimu - Sumba...



Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imewahakikishia wananfunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2018
kwamba watapata nafasi ya kuendelea na masomo yao huku Manispaa hiyo ikiendelea na juhudi za kujenga madarasa yanayohitajika.

Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Sumbawanga Silvester Mwenekitete alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya juhudi za manispaa 
kuhakikisha wanapambana na upungufu wa madarasa zaidi ya 18 yanayohitajika ili wanafunzi zaidi ya 2000 waendelee na masomo yao.

Amesema kuwa tayari Manispaa ya Sumbawanga imeagiza tani 90 za sementi kwaajili ya utekelezaji huona baada ya siku saba wanafunzi watakuwa na mahala pa kusomea 
ili waweze kutimiza ndoto zao.

"Madarasa yanajengwa katika shule mbalimbali, kizwite Sekondari madara matatu, Sumbawanga Sekondari manne, Katuma, matatu, kila mahali madarasa janajengwa na 
tumerekebisha madarasa natayari tuna madarasa ya kutosha, tayari halmashauri imeshaagiza tani 90 za simenti kwaajili ya madarasa haya na maandalizi ya mwakani 
na pia kuna bati kadhaa zipo njiani hii yote ni kusaidia nguvu za wananchi," Mwenekitete alimalizia.

Katika kushughulikia hilo timu maalum iliundwa na Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu ili kubaini mahitaji halisi kwa kila shule
kutoa mapendekezo na kuanza kuyashughulikia. ambapo hadi sasa madarasa 18 yapo tayari na wanafunzi zaidi ya 700 wameanza kusoma. 


Comments