Afisa Utamadunia wa Manispaa ya Sumbwanga Charles Kiheka amepania kuunda umoja wa wasanii wa maigizo katika manispaa ya Sumbawanga baada ya kutana na wasanii hao kwa lengo la kuwaelimisha namna ya kuweza kujisajili ili watambulike kisheria na kuisogeza Sanaa yao nje ya mipaka ya Mkoa nan chi kwa ujumla.
Amelifanya hilo baada ya kuona kuwa wasanii wengi wamekuwa
wakilalamika kuwa kazi zao hazithaminiwi na wanunuzi na kukosa ushirikiano kutoka
serikalini hivyo kupelekea maisha yao kuendelea kuwa duni licha ya kuipenda
kazi wanayoifanya kwakuwa wanajipatia kipato kupitia kazi hiyo.
![]() |
Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Charles Kiheka |
“Wasanii mmekuwa katika makundi makundi, hamna ushirikiano
katika kazi zenu, kila mtu ameonekana kujua kuliko mwengine, hampeani nafasi,
hamshauriani kwa mwendo huu hatuwezi kufika na kama tutafanya kazi kwa
ushirikiano tutakuwa mfano wa kuigwa n ahata halmashauri nyingine, Suluhisho
pekee mimi nitasimamia uundwaji wa umoja wa wasanii katika Manispaa hii.” Kiheka
alisem.
Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Ndugu Kiheka aliongeza
kuwa ni wakati sasa umefika wa wasanii kusahau tofauti zao na kushikamana kwa
pamoja ili kuhakikisha kuwa Sanaa ya Mkoa wa Rukwa inafahamika katika Nchi na
dunia kwa ujumla.
Picha ya pamoja wasanii wa maigizo wa Sumbawanga |
Nae kiongozi wa kikundi cha Sanaa cha Great Mind Association
(GMA) Frank Dachi aliunga mkono hoja ya Afisa Utamaduni huyo na kusema kuwa
kama wakongwe wa Sanaa wamepiti mengi na kati ya hayo hakuna faida waliyoiona
kwa wao kutengana zaidi ya kuongezeka kwa uhasama baina yao na hatimae kuanza
kugombea wasanii na kupelekea kazi zao kushindwa kuthaminika.
“Sisi wote ni watu wazima tumekuelewa Afisa, sisi tunaunga
mkono yale yote uliyoyasema a tunakuhakikishia kwa usimamizi wako kama
mwakilishi wa serikali kwenye hili tutafanikiwa, hapo mwanzo hatukuwa na
kiongozi kama wewe ambaye aliwahi kutukutanisha pamoja kama hivi, tunashkuru
sana,” Dachi alisem.
Kabla ya kumaliza mkutano huo Afisa Utamaduni aliweza
kuwateua watu wanne ambao watakuwa viongozi wa muda wa umoja huo hadi hapo
uchaguzi kamili utakapofanyika.
Comments
Post a Comment