 |
Afisa
Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Kiheka Charles akimkabidhi cheti
cha usajili wa kikundi cha Kwaya ya Mtakatifu Libori, Mwenyekiti wa
Kikundi hicho ndugu, Zenobius Ndelwa katika ofisi ya Utamaduni, Manispaa
ya Sumbawanga. |
Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga, Kiheka Charles amewaasa wasanii wa Manispaa ya ya Sumbawanga kujisajili ili waweze kutambulika kisheria.
Kiheka alihusia hayo alipokuwa akimkabidhi cheti cha usajili wa BASATA Mwenyekiti wa kikundi cha Kwaya ya Mtakatifu Libori chenye makazi yake katika kata ya Malangali ndugu Zenobius Ndelwa katika ofisi ya Utamaduni jengo la Manispaa ya Sumbawanga.
"Ni muhimu wasanii wote wajisajili ili wajijengee misingi ya kutambulika rasmi kiserikali na katika tasnia ya sanaa nchini. hii itawasaidia kuwajengea wigo mpana wa kufanya kazi ndani na nje ya nchi," Kiheka alisisitiza.
 |
Afisa
Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Kiheka Charles akimkabidhi cheti
cha usajili wa kikundi cha Kwaya ya Mtakatifu Libori, Mwenyekiti wa
Kikundi hicho ndugu, Zenobius Ndelwa katika ofisi ya Utamaduni, Manispaa
ya Sumbawanga. |
Comments
Post a Comment