Manispaa ya Sumbawanga kumaliza uhitaji wa madawati kufikia tarehe 15/09/2016


Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imepania kumaliza upungufu wa madawati ifikapo tarehe 15/09/2016, hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Manispaa Hamid Njovu alipokuwa akisoma ripoti ya madawati wakati walipokabidhiwa madawati 60 toka Tanesco.

Sambamba na hilo Ndugu Njovu aliomba wadau mbalimbali wa elimu nchini kuweza kuisaidia Manispaa kujenga vyumba vya madarasa 786 na matundu ya vyoo 1756.


Comments