134 wakamatwa Sumbawanga kwa kukaidi kufanya usafi wa mwisho wa Mwezi wa 7.





Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu.
Wananchi 134 wa kata mbalimbali za Manispaa ya Sumbawanga walikamatwa katika Jumamosi ya mwisho wa mwezi tarehe 30/07/2016 kufuatia kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika zoezi hilo.

Wananchi 131 walilipa fidia ya 50,000/= kila mmoja na Manispaa ya Sumbawanga kukusanya 6,550,000/= na wengine watatu kubaki katika kituo cha polisi kwa taratibu nyingine za kisheria. Wananchi hao walikamatwa katika kata ya Mazwi, Sumbawanga asilia, Maflala na katika kijiji cha Isesa kilichopo kata ya Mollo.

Katika kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kupitia Mh. January Makamba imetoa mwongozo wa maelekezo ya usafi wa siku hiyo ambao umechapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 22/04/2016 kupitia sheria yake ya usimamizi wa mazingira (The Environmental Management Act) sura ya 191 Kifungu cha 13 ibara ya 1,2 na 3.

Muongozo huo umeelekeza muda wa kufanya usafi kuwa ni kuanzia saa 12 hadi saa 3 asubuhi ambapo katika muda huo shughuli nyingine zote za kiuchumi au biashara zitasitishwa.

Comments