Wananchi 52 wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga watiwa
nguvuni baada ya kukaidi agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
John Pombe Magufuli la kufanya Usafi kuanzia saa 1:00 hadi 4:00 asubuhi kila
Jumamosi ya mwisho wa Mwezi.
Kati ya wananchi hao 52 ambao wengi ni wafanyabiashara ni 48
tu ndio waliofanikiwa kulipa faini ya shilingi 50,000/= kila mmoja na 2,400,000
zilikusanywa katika Mfuko wa mapato ya Manispaa, wananchi wane hawajalipa hivyo
faini na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu |
“Zoezi la Kufanya
Usafi ni la wananchi wote nchi nzima na hivyo ni wajibu wetu kutekeleza agizo
la Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli ili kuweza kuuweka mji wetu katika
mazingira safi na salama wa Afya zetu” Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga Hamid Njovu aliyasema hayo wakati alipoongea na waandishi wa habari
katika Ofisi za Manispaa.
“Wananchi hao walionekana kutojali agizo hilo na kuendelea
na Biashara zao huku wananchi wengine wakiendelea na Usafi katika maeneo mbali
mbali ya Mji wa Sumbawanga.” Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga alisema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu akiongea na Waandishi wa Habari |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu alisisita
na kutoa onyo kwa wale wote ambao watakaidi kwa jumamosi ya mwisho wa mwezi wa
saba kuwa watazunguka maeneo mengi Zaidi ili kuona zoezi hili linatiliwa mkazo
na wananchi wote wanashiriki kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli.
“Hatua kali za kisheria zikiambatana na faini na vifungo
mbali mbali itakuwa inatekeleza bila ya uwoga wala huruma na zoezi hili la
ukaguzi wa usafi wa maeneneo ya usafi na biashara itakuwa endelevu na wananchi
wote waendelee kuchangia gharama za uzoaji wa taka kwa mujibu wa sheria ndogo
za manispaa ya Sumbawanga.” Mkurugenzi Alimalizia.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Taka ngumu wa Halamashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamidu Masare |
Comments
Post a Comment