Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
imetoa shilingi Milioni 5 katika kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kata ya
kizwite ili kupata ofisi mpya itakayoweza kutoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo.
Ofisi hiyo ambayo imewekewa jiwe na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen alipofanya ziara ya kutembelea miradi
mbalimbali ya kimaendeleo inayofanywa na Manispaa ya Sumbawanga.
 |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu akitoa ufafanuzi juu ya ofisi mpya ya kata ya Kizwite. |
Katika kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo wananchi
walijichangisha Shilingi milioni 2.97 na wahisani wengine walitoa shilingi
100,000.
 |
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimsalimia Afisa maendeleo ya jamii wa kata ya Kizwite Sepe, alipotembelea katika kata hiyo ili kuweka Jiwe la Msingi katika ofisi mpya ya kata hiyo |
 |
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kizwite akisoma risala fupi ya ujenzi wa ofisi mpya ya kata ya Kizwite mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen. (jengo lenyewe lipo nyuma ya waheshimiwa waliokaa) |
 |
(Waliosimama kuanzia kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu wakimsikiliza kwa makini mwananchi David Msongole aliyeuliza juu ya swala la elimu bure na kutaka majibu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephenaliweza kumjibu vizuri juu ya taratibu zinazotakiwa kufuata katika kuendesha hilo suala la elimu bure. ikiwemo wananchi kuweza kutoa wazo la kuchangia mambo ya kimaendeleo katika shule za watoto wao bila ya upata ushawishi kutoka kwa watumishi wa serikali. |
Comments
Post a Comment