Katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli la kutotaka kusikia mwanafunzi anakaa chini
ifikapo tarehe 30, June 2016, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetumia
shilingi Milioni 50.8 kutengenezea madawati ili kuona Zoezi hilo linafanikiwa.
Pamoja na jitihada hizo Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga bado inakabiliwa na upungufu wa madawati 5,142 kwa shule za
Sekondari na Msingi huku asilimia 99 ya uhitaji huo ni katika shule za Msingi
za Manispaa hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina jumla ya shule za
Msingi za seriakali 55 na Sekondari 17, ambapo tangu mwaka huu uanze madawati
5,411 maptayari yameshatengenezwa na 1,367 yamekarabatiwa.
Mchumi wa Manispaa wa Sumbawanga Saad Mtambule alisema kuwa
changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha katika kufanikisha hili na Mvua nyingi
zilizonyesha mwezi Februari hadi Aprili zilisababisha mbao kutokauka mapema.
Lakini pamoja na Hayo Ng. Mtambule alisema “Pamoja na
Changamoto hizo kuna Jitihada kadhaa ambazo tunazifanya ili kukamilisha zoezi
ikiwemo kupasua mbao katika msitu uliyopo kwenye baabara ya kwenda Kasanga kwa
kibali cha TANROAD na pia kuendelea kupasua mbao katika miti iliyopo mashuleni”
Pia Mchumi wa Manispaa, Mtambule alongeza kuwa juhudi za
kuwashawishi wadau wa maendeleo bado zinaendelea na pia kutenga bajeti katika
mapato ya ndani ya manispaa ili kuweza ufanikisha Zoezi hilo.
Milioni 308.5 bado zinahitajika ili kufuta upungufu wa
madawati katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen(aliyevaa miwani) akiongozana na viongozi wenziwe kuangalia Madawati. |
Hivyo kama wewe ni Mdau wa maendeleo unaeishi Katika Masipaa
ya Sumbawanga usisite kuchangia ili wananfunzi ambao ndio Taifa la Kesho wawe
na Mazingira mazuri ya kupata Elimu.
Comments
Post a Comment