Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wapatiwa
mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa fedha ili kuwapa uwezo wa kusimamia vyanzo
mbalimbali vitakavyoongeza mapato katika manispaa hiyo.
Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa manispaa ya
Sumbawanga na kuendeshwa na katibu tawala wa serikali za mitaa kutoka ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mgonya.
![]() | ||
Katibu Tawala serikali za mitaa ndg. Albinus Mgonya akiendelea na mafunzo, |
Ndugu Mgonya alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea
ufahamu waheshimiwa madiwani ili kuweza kusimamia vyanzo vya mapato kwa
uangalifu mkubwa na kuwa, mafunzo hayo yametolewa kwa madiwani walio katika halmashauri
zilizo katika mikoa kumi nchini.
Vigezo vilivyotumika kuchaguliwa kwa mikoa hiyo ni pamoja na halmashauri zake kupata hati
zisizorisha, chafu au mbaya, pia halmashauri kutofanya vizuri katika makusanyo
yake ya ndani pamoja na mikoa yenye halamashauri mpya.
Wakati mafunzo hayo yakiendelea baadhi ya madiwani waliuliza
maswali mbali mbali li kuweza kupatiwa majibu na kuweza kujua nafasi zao na kutambua
majukumu yao kudhibiti mapato ya ndani ya halmashauri.
Mh. Vitalis Ulaya, diwani wa kata ya Msua alitaka kujua utoaji
wa taarifa za fedha ukoje, swali ambalo lilijibiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya
Sumbawanga ndugu. Hamid Njovu kwa kueleza kuwa kamati ya fedha hukutana kila mwezi
kupokea taarifa ya mapato na matumizi na hatimae kamati hiyo hutoa ushauri kwa
wataalamu wa manispaa inapoona inafaa.
![]() |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga ndg. Hamid Njovu akijibu swali. |
Kabla ya kumaliza mafunzo hayo ndugu Mgonya aliwasihi
waheshimiwa madiwani kuwahamasisha wananchi wanaowaongoza katika kata zao juu
ya kuchangia katika miradi mbalimbali ya kuendeleza halmashauri kupitia katika
kamati zao za maendeleo.
![]() |
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza mafunzo. |
“wananchi wanapokuwa wanachangia ile asilimia 2 ya mradi
huwafanya wanachi kuuona ule mradi kuwa ni wa kwao na kuweza kuulinda kwa nguvu
zote na kuuonea uchungu” Mgonya alisisitiza.
Comments
Post a Comment