Mitihani ya
kumaliza kidato cha sita mwaka 2016 yafanyika kwa Amani na kwa utulivu katika
halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Mitihani ilianza siku ya Jumatatu tarehe
2/5/2016 na kumalizika tarehe 11/5/2016. Jumla ya vituo ni 6 vyenye watahiniwa 612
waliosajiliwa, wakiwemo watahiniwa 450 wa shule na 162 wa kujitegemea.
Katika
kufafanua yaliyojitokeza afisa elimu sekondari Sylvester Mwenekitete alisema “Kwa
jumla hali ya mahudhurio ya watahiniwa ilikuwa nzuri. Hata hivyo, katika kituo
cha Msakila mtihani wa Advance Mathematics ilipelekwa lakini watahiniwa
hawakuwepo hivyo mitihani hii ilikabidhiwa kwa kamati ya uendeshaji wa mitihani
mkoa”
Miongoni mwa
shule zilizofanya mtihani huo ni Shule ya sekondari St. Maurus, Shule ya
sekondari Kizwite, Shule ya sekondari Kantalamba, Shule ya sekondari Msakila, Shule
ya sekondari Sumbawanga na Shule ya sekondari Aggrey Chanji.
![]() |
Walimu wa Shule ya Sekondari Sumabwanga |
Hakukutokea na
sifa yoyote ya wizi wa mitihani wala udanganyifu wa aina yoyote. Hii ilitokana
na umahiri wa ulinzi wa mitihani hiyo uliotolewa na jeshi letu la askari polisi
wa wilaya likishirikiana na kamati ya uendeshaji wa mitihani ya mkoa.
“ Nawatakia
kila la heri katika maisha yao ya baada ya shule ya Sekondari” Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kizwite
bwanaLazaro Mwandenene alitoa neno lake la mwisho kwa wanafunzi wote
waliomaliza salama mitihani ya kidato cha sita.
Comments
Post a Comment