Kama
ilivyokuwa kwa mpango wa BIG RESULT NOW (BRN) uliolenga kuboresha elimu nchini,
zoezi hili limegeukia upande wa sekta ya afya ili kuboresha utoaji huduma za
kiafya kuanzia ngazi ya zahanati kwenye kata hadi hospitali za wilaya.
Zoezi lilifanywa na timu ya utafiti kutoka wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,
wazee na watoto iliyoongozwa na Dokta Zuwena Bakari ikishirikiana na wahudumu
wa afya wa Manispaa ya Sumbawanga kupitia vituo vya afya 39 vya Mansipaa vikiwemo
vya serikali, mashirika ya dini na watu binafsi ili kujua uwezo wa vituo hivyo
kutoa huduma za afya.
Timu hii ya
utafiti iliyoundwa na watu 10 ilitumia siku 10 kupitia vituo vyote vya afya na
iliangalia mambo manne ili kuweza kutoa hadhi ya uwezo wa kituo, mambo hayo
yakiwemo idadi ya watumishi, utoaji wa tiba,utendaji kazi wa watumishi pamoja
na huduma wa afya ya uzazi kwa kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa
miaka mitano.
Hadhi hizo
zilitolewa kwa mfumo wa Nyota huku nyota tano ikimaanisha vizuri sana na nyota
moja bado sana na ambazo hazina nyota ikiwa na maana hazifai kutoa huduma mpaka
hapo mambo muhimu yatakapofanyiwa kazi.
Ni 72% ya
vituo hivyo ndivyo vilivyopata nyota 1 na 2 na 28% havikupata nyota hata moja,
jambo ambalo linahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee maana taifa bila ya watu
kuwa na afya nzuri haliwezi kujengeka.
![]() |
Dk.Zuwna bakari akitoa ufafanuzi wa ripoti |
“asilimia
kubwa ya zahanati hazina vyumba maalum vya kumchunguza mgonjwa kwa siri na pia
nyingi hazina magodoro na kupelekea wazazi wanaotaka kujifungua kulalia
misengela(mikeka) hali hii inasikitisha” Dokta Zuwena alisema.
Pia Dk.
Zuwena aliongeza kuwa 90% ya vituo hivyo havina umeme wa uhakika na kupelekea
watu kutumia vibatari na mishumaa jambo ambalo ni hatari kwani inaweza
kusababisha matatizo makubwa Zaidi.
Mbali na
hayo Dk. Zuwena alisikitishwa na ukosefu
wa maji wa asilimia 51 katika vituo walivyovitembelea na kuonya kuwa kama kama
magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu kinatokea uzuiwaji wake utakuwa mgumu
maana hata manesi watashindwa kutoa huduma ipasavyo.
Comments
Post a Comment