Waendesha Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wamewatandika bila ya huruma wahesabu fedha wa Benki ya NMB tawi la Sumbawanga magoli 3 -1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Nelson Mandela uliopo mjini Sumbawanga.
Magoli yote matatu ya Manispaa ya Sumbawanga yalipatikana Kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya wachezaji hao kupata maelekezo ya Kiufundi kutoka kwa kocha anaetambulika kimataifa Adam Evarist.
Goli moja la wahesabu fedha hao lilipatikana kwa penati baada ya Mchezaji wa Manispaa ya Sumbawanga kuunawa mpira.
Hapo awali kulikuwa na taarifa ya kuwepo kwa michezo miwili yaani mchezo wa mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa netiboli kwa wanawake lakini hadi mchezo wa mpira wa miguu kwa wanaume unakwisha wahesabu fedha hao wa kike hawakuonekana uwanjani jambo ambalo liliwahuzunisha waendesha Manispaa wa Kike, kwani walipania mchezo huo.
Mmoja wa viongozi wa wahesbu fedha alisema kwa uchungu kuwa atafanya juu chini mechi irudiwe ili waweze kuhamisha kilio katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Picha Zote na Irene Chale
 |
Comments
Post a Comment