Katika
kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli la kuhakikisha kuwa mpaka mwezi wa
sita mwaka 2016 hakutakiwi kuonekana mwanafunzi anakaa chini kwa kukosa dawati,
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imedhamiria kushirikiana na wadau wa
elimu ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu bora kwa kukaa katika
madawati katika mazingira bora.
Moja
ya kuhakikisha lengo hili kwani hatuwezi
kuwa na elimu bora wakati
watoto wetu wanakaa chini, wanakaa kwa
kubanana katika madarasa na kusoma katika madarasa yaliyo na vumbi.
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina Shule 72 za
serikali ikiwa 55 za Msingi na 17 za sekondari. Hadi sasa Manispaa ya
Sumbawanga ina wanafunzi 56,457 kwa shule za msingi ikiwa wavulana 27,039 na
wasichana 29,418.
Mfumo wa uendeshaji wa Elimu unaagiza uwiano wa dawati
1 kwa wanafunzi 3 hivyo kutokana na idadai ya wanafunzi 56,457 Halmashauri
inahitaji kuwa na madawati 18819 ila hadi sasa Halmashauri ina madawati 9484 na
kufanya upungufu wa madawati 9385.
Halmashauri imetoa pesa kiasi cha sh. 10,000,000/= kwa
ajili ya upasuaji mbao katika Maeneo Mbalimbali yaliyopandwa miti, maeneo hayo
ni kama vile katika Shule zetu za Msingi na Sekondari. Kupitia Miti hiyo Halamshauri inatarajia
kuvuna mbao zenye kipimo cha 1” x 8” x
10 kiasi cha mbao 3000 hadi 3500.
Halmashauri
imeagiza square pipe 1000 zenye thamani ya sh. 12,000,000/= ambazo zinaweza
kutengeneza fremu za madawati 500.
Halmashauri
imeagiza walimu wakuu kutumia 30% za fedha za capitation za uendeshaji wa shule
kwa ajili ya kukarabati madawati mabovu ili kupunguza uhaba huo. Na kupitia
Fedha hizo Halmashauri inatarajia kutengeneza Madawati 894.
Mfumo
wa uendeshaji wa shule za Sekondari unahitaji kuwepo kwa meza na kiti cha
mwanafunzi I kwa ajili ya Wanafunzi wa shule za Sekondari. Sekondari za
Manispaa zilikuwa zinahitaji Meza 4211 na viti 4211 Halmashauri ina upungufu wa
meza 1476 na viti 957.
Hivyo
ni jukumu letu kama wadau kuinua kiwango cha elimu katika Manispaa yetu ya
Sumbawanga kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na mazingira bora ya kufundishia na kusomea
watoto wetu.
Kwa
maelezo Zaidi piga simu kwa Mkurugenzi wa Manispaa 0624 777666
Au
tuma kwenye Akaunti ya NMB 62110001801
Comments
Post a Comment