Shule ya Msingi Kasisiwe yaongezewa madarasa matano.


Katika kukabiliana na wingi wa wananfunzi uliotokana na muitikio mkubwa wa sera ya elimu bure Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga inaendelea na ujenzi wa madarasa matano pamoja na ofisi moja ya waalimu katika shule ya msingi Kasisiwe.

Shule ya Msingi Kasisiwe

Mradi huo ambao utagharimu shilingi milioni 67.3 upo katika hatua ya kupiga plasta na tayari shilingi milioni 57.2 zimeshatumika na kutarajiwa kumalizika mwezi mei mwaka huu.

Kaimu Afisa elimu Msingi Manispaa ya Sumbawanga Frank Sichalwe amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutapunguza msongamano wa wanafunzi wanaosoma katika shule za Msingi Chanji, Utengule, Ndua na  Kizwite na Milanzi.

” Ujenzi ukikamilika utapunguza umbali kwa wanafunzi Kwenda shuleni, Wanafunzi na walimu kujifunza na kufundisha katika mazingira mazuri, Kuongeza tija ya ufaulu kwa wanafunzi kwa kusoma katika mazingira mazuri,” Alifafanua.

Hadi kukamilika kwa shule hiyo serikali kuu imechangia shilingi milioni 44.7, wananchi shilingi milioni 17.3 huku halmashauri ikiwa imechangia shilingi milioni 5.2.

Comments