Mtimbwa ‘B’ yaanzishwa kukabiliana na Elimu bure Sumbawanga


Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeanzisha ujenzi wa shule mpya ya msingi katika kata ya Matanga, Wilayani Sumbawanga ili kukabiliana na wingi wa wananfunzi walioandikishwa katika shule ya msingi Mtibwa kutokana na sera ya elimu bure iliyoanza mwaka wa masomo 2016.
Shule Mpya ya Msingi Mtimbwa, Sumbawanga. 

Shule hiyo mpya itakayoitwa Mtimbwa B tayari inaendelea na ujenzi wa madarasa saba yatakayogharimu shilingi milioni 75 ambapo hadi sasa milioni 56.6 imeshatumika na kubakia milioni 18.3 ili kumalizia ujenzi huo ulioanza mwishoni mwa mwaka 2017 na kutegemewa kumalizika mwaka huu.

Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amesema kuwa manispaa imeamua kuanzisha shule hiyo mpya ili kuboresha mazingira ya wananfunzi na walimu ya kujifunza na kufundishia pamoja na kuongeza tija ya ufaulu kwa wananfunzi kwa kusoma katika mazingira mazuri.

Akitoa mchanganuo wa fedha za ujenzi wa madarasa hayo Njovu alisema “Wachangiaji wa ujenzi huu ni serikali kuu amabayo imechangia 45,300,000 Halmashauri 15,000,000 pamoja na wanachi 14,700,000”

Ujenzi huo wa madarasa saba ya shule mpya ya msingi Mtimbwa B utapunguza mahitaji ya madarasa 801 yanayohitajika katika Manispaa ya Sumbawanga ili kuwa na madarasa 1309 yatakayotosheleza wananfunzi wa shule ya msingi 58,641 katika Manispaa.

Comments